Breaking News

DADA ZETU SIKU HIZI MNABOA SANA KWA HAYA MAVAZI YENU..!!



Habari zenu

Leo niko na nyie dada zangu ninaowaheshimu na kuwapa heshima mnayostahili!!

Ninakereka sana na vijivazi vyenu mnavyovivaa siku hizi kwa kuwa haviendani kabisa na utamaduni wetu wa kitanzania na unapoteza maadili kabisa katika jamii husika, siyo wakina dada wala akina mama, wote wamejisahau kabisa, unamkuta mdada/mama amekuvalia mini-skirt kiasi kwamba nusu kama siyo robo tatu ya maumbile yake anayaacha wazi,.

Sijui mnafanya makusudi ama vipi maana bado sijapata jibu mpaka sasa, wengine wanasema mnawatega wanaume ili waingie kingi, wengine wanasema ndiyo kuendana na wakati hivyo yaani ni taabu tupu dada zangu, kwanini msivivae hivi vijivazi mkiwa na mabwana zenu humo vyumbani kwenu muwaonyeshe neema mlizojaaliwa ili wawafurahie maana ndiyo wanaostahili kuyaona maumbile yenu?.


Badilikeni ili jamii iwarejeshee heshima yenu tafadhali!!!


BOFYA HAPO CHINI KUONA MFANO WA MAVAZI WANANYOVAA DADA ZETU SIKU HIZI...


Read more ...

VIDEO : MWANACHUO AFUMWA AKICHEZA NUSU UCHI KWENYE MTANDAO WA SKYPE BAADA KUDANGANYWA NA MZUNGU ALIYEKUWA ANACHAT NAE...




Huu ni mkasa wa mwanachuo wa kike aliyekutana na tapeli aliyejifanya yeyey ni mzungu yuko marekani.Baada ya kuzungumza kwa sms wakati wanachati ndipo mzungu huyo alipomuuliza mwanachuo huyo kama anaweza kuvua nguo na kucheza uchi huku akimwangalia kupitia webcam,na kisha kutoa ahadi ya kumtumia kiasi cha fedha baada ya mwanafunzi huyo kufanya hivyo.mwanachuo alifikiri anachati na mzungu kweli  kumbe alikua tapeli.kijana huyo alitumia uhuni wa kuweka picha ya mzungu ili aweze kumpata dada huyo kirahisi .Baada ya dada kukubali kucheza nusu uchi ,ndipo kijana huyo alimrekodi na kuposti video iyo ikimwonesha binti huyo akicheza nusu utupu

Video yenyewe hii hapa chini.....

                       
Read more ...

MWANAFUNZI WA CHUO KIKUU NCHINI AJIUZA KWA KUWEKA PICHA ZA UCHI KWENYE PROFILE YAKE YA FACEBOOK




Katika hali ya kushangaza msichana mmoja anaejiita Seche Mautamu ambae anajiuza kupita mtandao wa kijamii wa facebook kwa kuweka picha zake za utupu. Zifuatazo ni picha zake hizo na baada ya hizo picha utakuta link ya PROFILE yake ya facebook. Ukienda kwenye profile yake hiyo nenda kwenye About utaona AMESEMA anasoma CHUO ! Kama ni kweli ni mwanafunzi wa CHUO then taifa letu lina tatizo kubwa kuliko tunavyodhani.
Read more ...

BAADA YA PICHA ZAKE ZA UTUPU KUSAMBAA, WATU WAMPA MAKAVU LIVE MISS TZ REHEMA FABIAN...

MISS Kiswahili 2008 Bongo, Rehema Fabian amenagwa vibaya na wadau baada kutupia picha za utupu katika mtandao wa Instagram.
Rehema Fabian katika pozi.
Wakizungumza na paparazi wetu mara baada ya kuziona picha hizo ambazo zinamuonesha baadhi ya viungo vyake nyeti, mashabiki wa staa huyo walimponda wakidai wamemchoka kwa kupenda kupaisha jina lake kupitia picha hizo chafu.


“Anajidhalilisha sana, nahisi hajui thamani yake kwani mtu mwenye kujitambua hawezi kuweka picha zinazoonesha mwili wake ukiwa mtupu, asipo jirekebisha yatakuja kumkuta makubwa maana kila mmoja anaamini anajiuza,” alisema shabiki huyo aliyeomba hifadhi ya jina.

Rehema Fabian.
Shabiki mwingine aliyeona picha hizo mtandaoni, alichangia kwa kusema staa huyo hana lolote la maana analolifanya tangu atwae taji la u-miss zaidi ya kuweka picha za utupu kwenye mitandao ya kijamii.

“We kila siku habari zako ndiyo hizohizo, kwa nini usitafute kazi nyingine ya kufanya na kukuingizia kipato?” ilisomeka komenti hiyo katika mtandao wa Instagram.


Baada ya kupata malalamiko hayo ya kumponda Rehema kutoka kwa mashabiki tofauti, paparazi wetu alimcheki nyota huyo kupitia simu yake ya mkononi, alipopatikana alifunguka:
“Nimepiga mwenyewe na kuziweka katika ukurasa wangu, sasa nashangaa hao wanaosema eti najidhalilisha kwa lipi hasa?”
Read more ...

NAPENDA WAPENZI WA MTANDAONI ,ILA TUKISHA ''DO'' SIWAPENDI TENA...

Mimi ni Msichana wa Miaka 23 , muda mwingi nipo online kwenye Facebook ...sasa huko nimekuwa nikikutana na wavulana wazuri na huwa tunachat mambo ya mapenzi kama wapenzi .Mapenzi huwa matamu sana pale tunapochat na kufanya mapenzi online ila tukisha onana tu simpendi tena na ninatafuta mwingine online...Je nina tatizo ? nifanyaje niache?
Read more ...

Unajua athari za kuitana sweet, dear, baby katika mapenzi...?? SOMA HAPA NKUJUZE.



BABY ni neno la Kiingereza lenye maana ya mtoto, tena mara nyingi linatumika kwa mtoto mdogo. Pia lina maana nyingine ya mpenzi. Ni neno maarufu sana siku hizi; hata wazee kabisa, utasikia wanaitana baby!
Mbali na hilo, yapo maneno mengine kama sweet, dear, honey na mengine mengi. Maneno yote hayo ya Kiingereza, yana maana zaidi ya moja, lakini kubwa zaidi ni kumaanisha mpenzi, mpendwa (hutumika katika kuonesha mapenzi ya dhati kwa mwingine).
Leo nataka kukupa kitu kipya kabisa kichwani mwako. Unahitaji utulivu wa hali ya juu ili kujifunza hili. Ni maneno mazuri sana, ya kipekee lakini kwa upande mwingine ni hatari kwa sababu hukaribisha matatizo ambayo hayakutarajiwa na mtumiaji.


HUTUMIKA WAPI HASA?
“Dear, naomba uniamshe saa 12:00 asubuhi, kesho nina vikao vingi sana asubuhi,” inaweza kuwa kauli ya mume akimwambia mkewe, ambaye naye anamjibu: “Sawa sweet, usijali.”
Kwa hakika ndipo sehemu sahihi zaidi kutumika. Ni maneno yenye mshawasha mkubwa na huonesha penzi la dhati lililopo moyoni mwa mhusika kwenda kwa mpenzi wake.
Husisimua na kuongeza ladha ya mapenzi ya kweli. Kumuita mpenzi wako kwa majina ya kimapenzi huongeza zaidi upendo na msisimko wa moyo. Mwenzi hujiona wa kipekee na mapenzi huzidi kukua.
Kwa maana hiyo basi, ni sahihi zaidi kwa wapenzi kuitana majina niliyotaja hapo juu na mengine yanayofanana na hayo kwa lugha yoyote ile, ila iwe inatambulika vizuri na anayetamkiwa.


ATHARI SASA!
Kwa upande mwingine kuna athari za kutumia maneno hayo. Zama hizi, maneno hayo yanaonekana ya kawaida tu. Mtu yeyote anaweza kumuita yeyote mpenzi, honey, baby n.k. Hapo ndipo kwenye tatizo lenyewe.
Kwa ujumla wanawake ndiyo wanaongoza zaidi kuitana majina hayo. Wakati mwingine huenda mbali zaidi na kuwaita hata wanaume majina hayo ya kimapenzi. Si rahisi kuona athari zake kwa haraka na moja kwa moja, lakini zipo na wengi zimewasababishia matatizo. Ngoja tuone..


HUPUNGUZA THAMANI
Kama nilivyotangulia kusema awali, maneno 
niliyotaja hapo juu husisimua na kuongeza mapenzi. Kwa kuyatumia vinginevyo, basi kwa kiasi kikubwa huanza kukuathiri na kupunguza thamani ya neno lenyewe.
Kama unaweza kumwita mfanyakazi mwenzako dear, mtu wa jinsi sawa na wewe sweet ni wazi hata utakapomuita mpenzi wako au wewe kuitwa na yeye, halitakuwa na nguvu sana ya mapenzi kwa sababu ni neno ulilolizoea kila wakati.


HUKARIBISHA USALITI
Wakati mwingine unaweza kujikuta umeingia kwenye usaliti bila kutarajia. Veronica, mfanyakazi wa saluni moja ya kiume iliyopo Sinza, Dar alitoa ushuhuda ufuatao:
“Mimi naishi na mchumba wangu, tuna mtoto mmoja mwenye miaka mitatu. Nafanya kazi saluni. Tangu nimeanza hii kazi, nimejifunza kutumia maneno matamu ya kumfurahisha mteja na wakati mwingine kumfanya akupe tipu baada ya kumaliza kazi.
“Kuna kaka mmoja nilizoeana naye sana. Kama kawaida, huwa namkaribisha kwa kumuita dear au sweet. Wakati nikiendelea kumfanyia scrub, mazungumzo yetu hutawaliwa na dear, sweet, nikajikuta nimezidi kumzoea.
“Kwa sababu tulibadilishana namba, mara akaanza kuwa na mazoea ya kunitumia meseji, akija ananipa pesa, anaondoka. Mazoea yakazidi. Nikajikuta nimemzoea na kuna siku ambayo siwezi kuisahau kabisa.
“Ni siku niliyomsaliti mchumba wangu...mbaya zaidi na huyo jamaa naye ana mke wake. Niliumia sana, lakini naamini kama nisingekuwa na mazoea ya kumuita majina ya kimapenzi nadhani nisingeingia mtegoni. Moyo wangu unauma sana, najuta kumsaliti mpenzi wangu.”
Unaweza usione athari hii moja kwa moja, lakini ndugu zangu chukua jambo hili leo; wanaume wengi wakiitwa kwa majina ya kimapenzi husisimka sana – hujiona wenye bahati na mara hushawishika kuingia mapenzi.
Kama mwanamke hatakuwa makini atajikuta ametumbukia. Ya nini yote hayo, wakati unaweza kubadilisha mazoea hayo? 


ANGALIA TOFAUTI
Rafiki zangu, kati ya maneno niliyoyataja, kuna ambayo yanakubalika kutumiwa na wasio na uhusiano lakini wawe na undugu wa damu. Mathalani baba, mama, kaka, dada, shangazi nk.
Hakuna tatizo kumuita mtu mpendwa, lakini siyo baby, sweet, mpenzi na mengine yenye maana ya moja kwa moja ya kimapenzi. Umenipata? Akili za kuambiwa, changanya na zako kisha unazifanyia kazi! Chukua kinachokufaa
!

Read more ...

MWANAFUNZI WA KIDATO CHA KWANZA AFA MAJI SINGIDA

DSC07147 
Mwili wa mwanafunzi wa kidato cha kwanza katika shule ya sekondari Ipembe mjini Singida Rashid Said (16) (kushoto) na wa kijana ambaye hajafahamika jina aliyekuwa anajaribu kumwokoa mwanafunzi.Vijana hao wawili waliofariki dunia Machi 08 mwaka huu saa nane mchana ,mwanafunzi huyo amefariki dunia baada ya Mtumbwi waliokuwa wameupanda kupigwa na upepo na wao kutumbukia ndani ya maji.

DSC07161

Mwili wa mwanafunzi wa kidato cha kwanza shule ya sekondari Ipembe Rashid Said, ukiingizwa kwenye chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali ya mkoa mjini Singida.(Picha na Nathaniel Limu). 
MWANAFUNZI wa kidato cha kwanza katika shule ya sekondari ya Ipembe mjini hapa,Rashid Saidi (16) amefariki dunia baada ya mtumbwi aliokuwa umeupanda ziwani, yeye na baadhi ya wanafunzi wenzake kupigwa na upepo mkali na kusababisha mtumbwi kupinduka na wao kutumbukia kwenye maji.


Kijana mmoja ambaye sio mwanafunzi na jina lake bado halijapatikana,alijitolea kumwokoa mwanafunzi huyo,lakini naye kwa bahati mbaya alifariki dunia baada ya kunywa maji mengi na kuzama ziwani.Tukio hilo la kusikitisha limetokea machi nane mwaka huu saa nane mchana.


Inadaiwa kuwa wanafunzi hao baada ya kumaliza kipindi cha’tuition’ shuleni kwao,kama kawaida yao walienda ‘pikiniki’ katika ziwa la Kindai na kuanza kuogelea pembeni mwa ziwa hilo.


Askari kutoka kikosi cha zima moto mjini hapa,Bahati Hemed,amesema kwa mujibu wa taarifa alizopewa na mashuhuda wa tukio hilo,ni kwamba baada ya wanafunzi hao kumwagwa ndani ya maji,baadhi ya wanafunzi walifanikiwa kujiokoa na Rashid ambaye hana uzoefu wa kuogelea,alizama nada ya maji.


Amesema wanafunzi hao baada ya kutoka nje ya ziwa,walimwomba kijana mmoja ambaye alikuwa na umri mkubwa aingie ziwani ili akamwokoe mwanzao.


“Yule kijana aliyejitolea kumwokoa mwanafunzi, alipokaribia alikotumbukia mwanafunzi huyo, na yeye mambo yalimwendea vibaya na hivyo kutupikia ndani ya maji na kusababaisha na yeye apoteze maisha yake”alisema Bahati kwa masikitiko.


Alisema baada ya hapo waliweza kuita wavuvi ambao walifika na nyavu na kuwaza kutoa miili hiyo miwili kutoka ndani ya ziwa Kindai.
Read more ...

USIYO YAJUA KUHUSU Z-ANTO:FAHAMU MAISHA YAKE BAADA YA MKEWE BINTI KIZIWI KUKAMATWA NA MADAWA YA KULEVYA NA KUFUNGWA NCHINI CHINA

ZANTO
Sababu za kupotea kwake;
Ukiongelea jina kama Z-anton kwa wengi watakuwa wanamjua msanii huyu maarufu kwa wimbo wake uitwao binti kiziwi,unaweza kusema kuwa ni moja ya waasisi wa muziki huu wa bongo fleva, ambao wameweza kukusanya wapenzi wengi wa muziki huu wa bongo fleva,nakuweka mchango mkubwa katika kukuza muziki huu na kufanya uweze kupendwa na mashabiki wa kila rika…na kama ulikuwa unajiuliza huyu mtu yuko wapi,.. he is back! anakuja tena na nguvu mpya hivi sasa katika game hili la muziki wa bongo fleva.

Akiwa anahojiwa na kipindi kimoja cha television nchini Kenya amefunguka nakusema kuwa upotevu wake katika game la muziki huu,ni kutokana na matatizo ya hapa na pale yakifamilia na kibinafsi zaidi aliyokuwa anakabiliana nayo,ila kwa hivi sasa its all gud,yuko teyari kurudi kwenye game.
Kuhusu muziki wake;
Kuhusu muziki anafunguka na kusema kwa sasa amerudi katika game na nguvu mpya kabisa,ingawa kulikuwa na baadhi ya watu waliokuwa wanamwekea vizingiti ili asiweze kurudi katika game hili la bongo fleva,ila kwa hivi sasa anarudi kipekee zaidi,hii yote ni baada ya kujitoa katika kundi lake la zamani la tiptop connection na kuongezea kuwa hana mpango hata wakurudi kundini cause anataka kufanya masuala yake ya muziki mwenyewe,bila ya kutegemea mkono wa mtu yeyote Yule kwa hivi sasa.
Maisha yake ya mahusiano baada ya binti kiziwi kukamatwa;
Rumors zilikuwa za kweli kwamba mpenzi wake aliyekuwa amekamatwa huko nchini china amefungwa kutokana na kosa la kuingiza madawa ya kulevya,na zaidi ni kuwa huko aliko anatumikia kifungo cha miaka sita,ila kwa upande wa Z-anton, hayo yote hayamhusu kwa sasa ,cause walishatemana siku nyingi na habari ya mujini ni kwamba hivi sasa anampenzi mwingine ambaye wamefanikiwa kupata mtoto mmoja.
Read more ...

JE WAJUA SIMU YAKO YA MKONONI YAWEZA SABABISHA UKAZAA MTOTO MTUKUTU...?? SOMA HAPA


MIONZI ya simu za mkononi inaweza kuathiri maendeleo ya ubongo wa watoto walioko tumboni mwa mama zao, utafiti umeeleza.Utafiti huo umetaja madhara mengine ya mionzi ya simu za mkononi kuwa ni uharibifu wa manii, mimba, kupungua kwa nguvu za kiume, kupoteza kumbukumbu na kuzaa watoto watukutu.

Pia umeeleza kuwa matumizi kupita kiasi ya simu hizo, husababisha mtindio wa ubongo na upungufu wa udadisi kwa watoto tangu udogo wao.

Hata hivyo, utafiti huo uliofanywa na Shule ya Tiba na Dawa ya Chuo Kikuu cha Yale, Marekani na kuripotiwa na Gazeti la The Telegraph la Uingereza, umepingwa na watafiti wengine, wakisema haujakidhi baadhi ya vigezo ili kuuthibitisha.
 
Kiongozi wa jopo la utafiti huo, Profesa Hugh Taylor alisema utafiti huo ulioanzia kwa panya, baadaye ulithibitika kwa binadamu.

Profesa Taylor ambaye pia ni Mkuu wa Idara ya Uzazi, Magonjwa ya Wanawake na Sayansi ya Uzazi, alisema: “Tulikuwa na panya wenye mimba katika maboksi na tuliwawekea simu juu ya vichwa vyao. Panya tuliokuwa tumewaweka katika bwawa lile, nusu yao walikuwa wazima na nusu yao walikufa. Panya waliokuwa hai tuliwaacha wajifungue na baada ya kujifungua, tukaanza kutafiti watoto wao.”
 
“Panya ambao hawakuwa karibu na simu za mikononi walionekana kuwa werevu. Kumbukumbu zao hazikupungua ikilinganishwa na panya walioathiriwa na mionzi ya simu za mikononi ambao katika vipimo vya awali wakiwa tumboni, walionekana kuhangaika.”

“Panya hao wenye mimba waliowekwa kwa siku 17 katika boksi hilo na simu kupigwa mfululizo juu ya vichwa vyao, walizaa watoto watukutu na waliokosa kumbukumbu.”
 
Aliongeza: “Matokeo hayo yanaweza kutokea kwa binadamu pia. Mjamzito anayetumia simu ya mkononi muda mwingi, anaweza pia kuzaa taahira.”

Utafiti huo umebaini kuwa kati ya asilimia tatu na saba ya watoto wenye umri wa kwenda shule, wana tatizo la utukutu linaloweza pia kuathiri maendeleo yao kitaaluma. Alisema kiwango hicho kimekuwa kikiongezeka kwa asilimia tatu kila mwaka tangu mwaka 1997.
 

Profesa Taylor alisema anaamini kuwa simu za mikononi pia ni sababu ya baadhi ya watoto kukosa adabu na pengine kutokuwa makini katika mambo mbalimbali wanapokuwa watu wazima.
 

“‘Huu ni utafiti wa kwanza unaoonyesha ushahidi wa madhara ya mionzi ya simu za mkononi. Tumeonyesha kuwa matatizo ya tabia katika panya yalitokana na mionzi ya simu za mkononi waliyoipata wakiwa tumboni,” alisema Profesa Taylor na kuongeza:
 

“Kuongezeka kwa utovu wa nidhamu kwa watoto kunaweza kuwa sehemu ya madhara ya mionzi ya simu, ambazo mama zao walikuwa wakizitumia wakati wao wakiwa bado tumboni.”
 

Profesa Taylor alifanya utafiti huo kwa kuwachukua panya 33 wenye mimba na kuwaweka kwenye boksi lenye nyavu kisha kuweka simu juu yake. Simu hiyo ilikuwa ikiita mfululizo kwa siku 17.
 
Pia aliwaweka panya wengine 33 katika mazingira ya aina hiyo lakini hakuweka simu juu ya boksi hilo.
“Zaidi ya watu 160 waliofanyiwa utafiti wa aina hiyo pia walionekana kuwa na tofauti za kitabia ambayo inaweza kuhusishwa na utafiti huo.

Hata hivyo, Profesa Taylor alisema kuna haja ya kuendelea kufanya utafiti zaidi ili kubaini sababu ya mionzi hiyo ya simu kuathiri watoto walio tumboni mwa mama zao na namna bora ya matumizi ya simu kwa wanawake wajawazito.
 

Mtaalamu huyo anatarajia kuungana na wenzake akiwamo Dk Devra Davis, anayeongoza Shirika lisilo la Kiserikali la Mazingira na Afya la “Environmental Health Trust” kwa ajili ya utafiti zaidi kuhusu madhara ya simu.
 

Mwaka 2011, Shirika la Kimataifa la Afya Duniani linalojihusisha na uchunguzi wa kansa, lilidai kuwa mionzi ya simu inaweza kusababisha kansa na hivyo jopo hilo la madaktari linaendelea na utafiti zaidi.
 

Nchi nyingine duniani ikiwamo Ufaransa, ilipiga marufuku kwa kampuni za matangazo ya simu kwa watoto kutokana na hatari mbalimbali zinazoweza kuwatokea.
 

Utafiti huo uliochapishwa katika Jarida la ‘Scientific Reports’ wiki iliyopita
 
Lengo la utafiti
Ongezeko la matatizo ya magonjwa wa mishipa ya fahamu, matatizo mbalimbali ya ubongo pamoja na magonjwa ya akili, ni mojawapo ya mambo yaliyochagiza kufanyika kwa utafiti huo.
Dk Hugh alisema simu za mkononi hazina madhara kwa watu wazima kama inavyodaiwa na wengi, lakini ni vifaa vyenye kuleta athari kubwa kwa watoto walio tumboni.

“Matatizo yanayowapata watoto wa binadamu walio wengi hivi sasa ikiwa ni pamoja na magonjwa ya mtindio wa ubongo, mishipa ya fahamu inasababishwa na matumizi ya simu za mkononi kwa mama wajawazito pamoja na kukaa nazo jirani kwa muda mrefu.”
 

“Haijalishi mama anaongea na simu au la! Mionzi inapenya na kuleta madhara pia kusababisha kazi ya ukuaji wa mtoto katika ubongo kulegalega, wapo ambao wanalala na simu kitandani zikiwa zimewashwa... hii ni hatari zaidi labda iwe imezimwa,” anasema Dk Hugh.
 

Watalaamu Dar
 
Akizungumzia utafiti huo jana, Mkurugenzi wa Teknolojia ya Nyuklia wa Taasisi ya Mionzi Tanzania (Taec), alisema ni vigumu kuukosoa utafiti huo kwa sasa hadi hapo Shirika la Afya Duniani (WHO), litakapotoa tamko sahihi ingawa alisema mionzi ina athari kubwa kwa binadamu.

“Nilipata kusoma utafiti huo katika mitandao siku mbili zilizopita, ni utafiti ambao umewekwa wazi, kwa kweli hata mimi ulinishtua, lakini ni mapema kuzungumzia hilo kwa sasa. Kwani utafiti huo bado unakinzana kwa mambo mengi, licha ya kupingwa pia na baadhi ya wanasayansi.

“Nadhani ni muda mwafaka sasa kufanya uchunguzi kwa binadamu na si kutumia panya kama walivyofanya Chuo Kikuu cha Yale. Hata hivyo, jopo la madaktari pia wanatarajia kufanya kikao chao mapema wiki hii, labda tutapata maoni mapya.”
 

Alisema kwa kawaida mionzi ina madhara kwa binadamu, lakini bado kuna maswali mengi kwa wanasayansi duniani ambayo bado hayajapatiwa ufumbuzi, hivyo inawawia vigumu Taec kutoa ufafanuzi wowote kuhusu athari hizo.
 


Meneja wa Mawasiliano wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Innocent Mungy alisema utafiti huo unaweza kuwa msaada mkubwa kwa nchi kama Tanzania ambayo hivi sasa ndiyo imechipukia katika matumizi ya simu za mkononi.
Read more ...

Aibu! Mke wa mtu anaswa wizi wa vitenge….!!

ANGEL Zambi ambaye ni mke wa mtu, mkazi wa Kitongoji cha Ipogolo mjini Iringa amenaswa akiiba vitenge na kanga kwenye duka moja, Risasi Mchanganyiko linakupa ‘ei tu zedi’.
Tukio hilo la aibu lilijiri Jumatatu iliyopita saa 5:10 asubuhi kwenye Mtaa wa Uhindini mjini Iringa jirani kabisa na Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Usharika wa Kanisa Kuu.

Wakizungumzia tukio hilo, baadhi ya mashuhuda waliliambia gazeti hili kwamba, siku ya tukio, mwanamke huyo akiwa na wenzake watano walifika katika duka hilo la Elizabeth Mlowe kama wateja wa jumla wa nguo.

“Walimkuta binti muuzaji,  wakaanza kumsumbua kwa kuagiza nguo bila mpangilio, yule anaagiza aina ile  huku mwingine akiomba kusogezewa vitenge na kanga. Hali hiyo ilimchanganya muuzaji na kujikuta akiibiwa kirahisi na Angel,” alisema shuhuda mmoja.
vite

Akihojiwa na paparazi wetu, mwanamke huyo mwenyeji wa Mbeya aliyeolewa Iringa alisema kuwa alijiunga na mtandao wa wizi kwa kuzunguka madukani siku mbili zilizopita (Jumamosi).

Alisema kuwa mtandao huo unajulikana kwa jina la Zubaa Tutajirike (Zutu), upo Ipogolo kwa sasa lakini ulianzishwa jijini Mbeya ila baada ya kugundulika mbinu yao walihamia Iringa na kuendelea na wizi huo.
“Kwa kweli najuta sana,   ni mara yangu ya kwanza kuingia katika kazi hii hapa Iringa, wenzangu ambao wamenikimbia wao ni wenyeji. Mume wangu alinikataza kutembea nao, ila leo nimemtoroka,” alisema kisha kupelekwa polisi mjini hapa.
Read more ...

MKE: NILIOLEWA ILI NIAMBUKIZWE UKIMWI...!! SOMA MKASA HUU WA KUSIKITISHA

UKISIKIA simulizi ya Hafsa Ramadhani (19) itakutia simanzi, itakutesa moyo na kukutoa machozi, huwezi kuamini aliingia kwenye ndoa bila kujua kuwa alikuwa akienda kukutana na ugonjwa wa ukimwi, Risasi Mchanganyiko linakufunulia.
Hafsa Ramadhani.
Habari kutoka chanzo chetu cha kuaminika zinasema, binti huyo alifanyiwa mipango ya ndoa bila yeye na mumewe huyo kupima kwanza maambukizi ya ugonjwa huo, ingawa tahadhari hiyo ilitolewa mapema kwa kuwa muoaji alikuwa akijulikana kuwa aliishi na ugonjwa huo kwa muda mrefu.
ILIKUWAJE?
“Huyo binti alitokea Bukoba, akaja hapa Dar es Salaam kutafuta kazi. Akaanza kufanya kazi za ndani, akiwa mdogo kabisa. Alihangaika kwenye nyumba mbalimbali lakini baadaye akafikia kwenye kituo cha watoto yatima (kwa sasa tunahifadhi jina), kipo Charambe ambapo alianza kuishi hapo,” kilipasha chanzo chetu kwa sharti la kutotajwa jina lake gazetini.
“Alipofikisha umri wa miaka 15 tu, wale watu wa pale kituoni wakamuozesha kwa jamaa mmoja (jina tunalo) ambaye kwa sasa ni marehemu. Huyo jamaa alikuwa akiishi na VVU na mbaya zaidi, hao watu wa hapo kituoni, walishauriwa kuhusu jambo hilo wakapuuza, ndiyo maana wengi wanaamini walimfanyia makusudi,” kilieleza chanzo hicho ambacho kimedai kipo karibu na binti huyo.
HUYU HAPA HAFSA
Timu ya gazeti hili kwa msaada wa chanzo chetu, ilifanikiwa kukutana na Hafsa ambaye kwa mwonekano ni binti mdogo na mpole kiasili, akazungumza mengi yanayomsibu katika maisha yake.
“Sikujua kama maisha yangu yangeishia hivi. Sikutegemea kama ningeteseka kiasi hiki. Kwanza mimi sijawahi kuwaona wazazi wangu. Niliambiwa tu walikufa tangu nikiwa mdogo, kwa hiyo nilikulia kwa wazazi wa kufikia huko Bukoba,” anaanza kusimulia Hafsa.
Akaendelea: “Baada ya kuolewa, maisha yalikuwa ya shida sana. Nilichukuliwa hapa Dar na kwenda kuishi na huyo mume wangu Arusha baada ya kufunga naye ndoa. Alikuwa haniachii fedha ya matumizi wakati mwingine lakini hali yake ya kuugua kila mara iliniogopesha ingawa sikuwahi kufikiria kabisa suala la ukimwi.
“Nilibahatika kupata mtoto na huyo bwana na hapo ukawa mwanzo wa mimi kuanza kuugua mfululizo. Nikiwa bado naumwa, mume wangu alifariki dunia. Basi, maisha yangu yakazidi kuwa magumu maana sikuwa na msaada wowote.”
DOKTA AMWAMBIA UKWELI
“Nikiwa nakwenda kliniki huku afya yangu ikiwa si ya kuridhisha, daktari mmoja alinishauri nifanyiwe vipimo. Ilibidi nishauriwe sana kabla ya kupimwa na kwa bahati mbaya nikagundulika kuwa nina ukimwi. Hata mwanangu pia ameathirika.
“Najua walinificha kwa muda mrefu kutokana na umri wangu, maana sasa nina miaka 19 na mwanangu mitatu, kwa hiyo wakati najifungua nilikuwa na 16 tu. Naiona dunia chungu kwa kweli.”
MAISHA MAGUMU ARUSHA, ARUDI DAR
“Kutokana na maisha ya mateso ya ndugu wa mume wangu kule Arusha, nilijikusanya nikapata nauli, nikaamua kutoroka na kurudi zangu Dar. Sikuwa na mahali pengine pa kwenda zaidi ya kurudi kituoni nilipokuwa nalelewa.”
ANYANG’ANYWA MWANAYE
“Mwanangu ndiye alikuwa faraja yangu pekee lakini wakwe zangu walikuja kuninyang’anya mtoto wakisema eti sina uwezo wa kumlea. Kwa kuwa ni damu yao, sikuwa na jinsi ikabidi nikubali tu. Sasa hivi anaishi nao huko Temeke.
“Nashukuru Mungu, nilipata msamaria (aliomba asitajwe jina lake) ambaye aliguswa na ugumu wa maisha yangu, akanikaribisha nyumbani kwake. Naishi naye Mbagala – Zakheem (Dar), lakini nina ugumu wa maisha. Kama unavyojua, siwezi kumtegemea yeye kwa kila kitu.”
ANAHITAJI MSAADA WAKO
Kama umeguswa na kisa cha Hafsa na ungependa kumsaidia kwa hali na mali, unaweza kufanya hivyo kwa kutumia namba 0783 855453 au 0713522779.
Read more ...

HIKI NDIO KISA CHA MSANII NAAZIZ WA KENYA KUMTOSA MUME WA KITANZANIA



Mwanadada Naaziz wa Kenya ambaye ni msanii wa siku nyingi na alikua mmoja kati ya waanzilishi wa muunganiko wa wasaniii wa Africa mashariki (East African Bashment Crew) pamoja na crew ya wasanii watatu wa Kenya Ndani yake akiwemo Wyre pamoja na Bamzigi, kwa miaka karibu mitano ameishi ndani ya ndoa na Mtanzania 

Member wa kundi la Necessary Noise la Kenya na East Arican Bashmen Crew Nazizi Hirji amethibitisha kutengana na mume wake baada ya ndoa yaoambayo imedumu kwa takribani miaka mitano. 

Baada ya kusambaa kwa taarifa hizo Nazizi amethibitisha juu ya taarifa hizo alipofanya mahojiano na moja ya kituo cha Nairobi na kuongeza kuwa hawezi kutoa taarifa zaidi lakini ifahamike ni kweli ndoa yao imefikia ukingoni.

Nazizi na aliyekuwa mume wake walifanikiwa kupata motto mmoja wa kiume ingawa bado wanaendelea kuzungumza licha ya ndoa yao kuvunjika.

Credit: Bongoclantz
Read more ...

KIM KARDASHIAN ANUSURIKA KUFA, APATA AJALI YA GARI



WAKATI akiwa katika maandalizi ya harusi yake mwanamitindo ambaye pia ni mchumba wa msanii wa Hip Hop nchini Marekani Kim Kardashian jana alipata  ajali ya gari ambayo haikuwa na madhara makubwa wakati akiendesha gari lake aina ya Mercedes G Wagon na kukwaruzana na Nissan Sentra.

Hata hivyo, gari la Kim Kardashian halikuharibika zaidi mkwaruzo mdogo iliupata lakini Nissan Sentra inadaiwa kuharibika vibaya sehemu ya mbele.

Shuhuda wa tukio hilo ameiambia TMZ kuwa Kim Kardashian alikuwa anakata kona kuelekea kushoto wakati dereva wa gari aina ya Nissan alikuwa anaonesha ishara ya kuelekea kulia, lakini kwa bahati mbaya badala ya kulekea kulia alinyooka na barabara na kulifikia gari la Kim K na kusababisha magari hayo kukwaruzana.

Imeelezwa kuwa wawili hao waliendesha hadi Beverly Hills Hotel ambapo walizungumza na kuyamaliza na kila mmoja akaendelea na safari yake bila polisi kuhusika.
Read more ...

UCHAWI:MWALIMU MKUU SHULE YA MSINGI AKIWA NA NGUO YA NDANI AMELALA KWENYE KIBAO CHA SHULE.


 



MWALIMU Mkuu wa Shule ya Msingi Rutamba, Wilaya ya Lindi amekutwa akiwa na nguo za ndani pekee katika usingizi mzito kwenye kibao cha shule hiyo huku akiwa hajitambui kwa madai ya kilichomkutana kinahusishwa na imani za kishirikina.
Tukio hilo limetokea juzi usiku baada ya mkazi mmoja wa kijiji hicho, Juma Mbilemoto kumkuta mwalimu huyo akiwa kwenye kibao hicho wakati alipokuwa anamsindikiza nduguye,Aisha Mbilimoto aliyekuwa anasafiri kuelekea Dar es Salaam.
Akizungumzia tukio hilo, shuhuda huyo alisema alimkuta mwalimu huyo akiwa amelala chini ya kibao cha shule akiwa na nguo ya ndani tu (chupi)huku akikoroma kutokana na kuwa na usingizi mzito.Alisema awali hakumtambua mtu huyo lakini baada ya kumkaribia alimtambua kuwa alikuwa mwalimu mkuu wa shule hiyo na ndipo alipochukua jukumu la kumwamsha  ili amvalishe kanga, lakini aliikataa na kuondoka kwenda nyumbani kwake akiwa kama alivyokutwa
Kwa upande wao walimu wa shule hiyo walisema kuwa, wamekosa molari wa kufanya kazi kutokana  na kitendo alichofanyiwa mwalimu mwenzao.
Akizungumza kwa niaba ya walimu wenzake mwalimu wa taaluma wa shule hiyo, Francis Milanzi alisema  walimu shuleni hapo wamekosa amani na kuwasababishia kuzihama nyumba zao  kwa muda na badala yake kwenda kukesha  kwenye ofisi za walimu tangu tukio hilo litokee.
Ofisa elimu wa Wilaya ya Lindi, Cosmas Magigi alisema amepokea taarifa za tukio hilo kwa huzuni na amewaomba walimu kuwa na subira wakati utaratibu wanalishughulikia suala hilo.
Magigi aliongeza kuwa ofisi yake itafanya utaratibu wakumhamisha  mwalimu huyo na kumtafutia shule nyingine huku akiwataka wakazi wa eneo hilo kujenga ushirikiano na watumishi ili waweze kutekeleza majukumu yao.
Hili ni tukio la pili kutokea katika halmashauri hiyo mwaka huu ambapo la kwanza lilitokea April katika Shule ya Sekondari Ruhokwe, mwalimu wa shule hiyo alilazwa kwenye kibao cha shule  akiwa uchi wa mnyama.
Read more ...

USHOGA BONGO MOVIE WATAWALA:WAANZA KUFICHUA SIRI WASANII WENYEWE JUU YA KUSAMBAA KWA USHOGA NDANI YA BONGO MOVIE

IMEBAINIKA kuwa ndani ya tasnia ya filamu Bongo kuna baadhi ya wasanii wanaofanya mapenzi ya jinsia moja yaani mashoga, Risasi Mchanganyiko limenyetishwa.
Mwenyekiti wa Bongo Movie Unity, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’.
Hilo limeibuka ikiwa ni siku chache baada ya Rais wa Uganda, Yoweri Museven, kupitisha sheria nchini mwake ya kupiga marufuku mavazi yasiyo na staha, uvunjifu wa maadili na mapenzi ya jinsia moja.
Uganda ipo katika Jumuiya ya Afrika Mashariki ikiunganishwa na nchi za Tanzania, Kenya, Rwanda, Burundi na Uganda yenyewe.
HABARI KAMILI
Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali vilivyomo ndani ya kundi hilo, baadhi ya wasanii wa kiume wanadaiwa kuwa ni mashoga, ingawa wanajifanya vidume vya mbegu.
“Wapo mashoga na mabwana zao tunawajua ila sema sasa kwa sababu huna ushahidi wa moja kwa moja na hujamfuma kwenye tukio, unashindwa kumtaja,” alisema msanii mmoja wa kike, Bongo.
“Yule…(analitaja jina la msanii mkubwa) bwana’ke alifariki na sasa ana mwingine lakini ndani ya Bongo Muvi anaonekana kiwembe kwa sababu ana msururu wa wanawake,” alisema.
AMSHAURI JK
“Ingekuwa vyema sana kama Rais Jakaya Mrisho Kikwete akafanya kama alivyofanya mwenzake wa Uganda, Yoweri Museven katika kupiga vita ushoga,” alipendekeza msanii huyo.
Msanii mwingine wa kike ambaye amekuwa kwenye tasnia hiyo tangu enzi za makundi ya sanaa kutamba runingani (jina kapuni) naye alikiri kuwepo kwa ishu hiyo lakini akadai wanafanya kwa siri sana.
“Kuna wasanii wanaonekana watanashati mbele ya jamii lakini ni chakula ya watu kwa kuwa wanapenda sana vitu vya bure,” alisema msanii huyo na kuongeza:
“Wapo wengi tu ndiyo maana katika maisha yangu sijawahi kutoka na mwanaume wa Bongo Muvi, ni wachafu sana. Siku zote wasanii wa kike ndiyo tunaoambiwa kuwa ni malaya, eti tuna tamaa na habari nyingi zinatuchafua siye lakini ukweli ni kwamba hata wanaume wana tamaa ya maisha mazuri na mwishowe wanageuzwa wanawake.”
HUYU YUPO TOFAUTI NA WENZAKE
“Sikia nikuambie, ni kweli hili suala lipo lakini si kwa wote na kuna baadhi huwa wanasingiziwa tu. Unajua nini? Unaweza kukuta mtu ana tabia tu ya kujipenda, lakini wengine wanasingizia kuwa eti ni mashoga – siyo kweli.
“Mfano hata uje na greda hapa, akitokea mtu anazungumza upuuzi eti JB, Dk. Cheni, Ray, Hemed PHD, Mlela au Dude ni mashoga, nitabishana nao mpaka mwisho. Hao ni watu ambao wanajipenda tu, sasa ukiwahusisha na huo ujinga nitashangaa sana. Sisemi kuwa wanatajwa ila sasa akitokea mjinga akaja na hoja hiyo, nitabishana naye,” alisema msanii mmoja ndani ya Bongo Muvi.
Msanii Hisani Muya ‘Tino’ aliwahi kuigiza kama shoga na kusababisha minong’ono kwenye jamii, katika filamu aliyoipa jina la Shoga lakini ilizuiwa na serikali.
Mwingine ni Dk. Cheni ambaye amecheza kama shoga kwenye filamu yake ya Nimekubali Kuolewa, ingawa bado haijatoka mpaka sasa.
Msanii huyo akizungumzia hayo, alisema: “Kucheza filamu kama shoga hakuna maana kuwa kweli ni shoga, ni kuvaa uhusika tu. Watu wasiwahusishe wasanii walioigiza kama mashoga kwenye hii skendo,” aliweka nukta msanii huyo mwenye maneno mengi.
WASIKIE WENYEWE
Baada ya kupata taarifa hizo, waandishi wetu waliwatafuta baadhi ya wasanii wa kiume Bongo wanaotesa na kuwauliza kuhusu ishu hiyo (wasanii hao hawamo kwenye orodha tuliyonayo).
Wa kwanza kuzungumza alikuwa ni Mahsein Awadh ‘Dk. Cheni ambaye alisema: “Miye sina la kusema kuhusu hilo, ni vyema kama utamtafuta mwenyekiti (Bongo Movie Unity, Steve Nyerere) ndiye mwenye mamlaka ya kuzungumza masuala kama hayo.”
KULWA KIKUMBA ‘DUDE’
“Hilo suala la ushoga ndani ya Bongo Muvi lipo hata miye nalisikiasikia, lakini halina uthibitisho ila kusemwa linasemwa sana.”
STEVE NYERERE
 
Mwenyekiti wa Bongo Movie Unity, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’: “Ni kweli taarifa hizo zipo, wasanii wakishakunywa pombe huwa wanafanya mambo ya ajabu sana kuashiria tabia zao halisi, mimi kama mwenyekiti wa Bongo Movie huwa ninaumia sana.
“Nitahakikisha nawafukuza mashoga wote hata kama tutabaki wawili katika kundi letu, bora wawe na heshima.”
MWAKIFWAMBA SASA
Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania ‘TAFF’, Simon Mwakifwamba: “Hiyo ishu ni kweli ipo, ndani ya Bongo Muvi, mashoga wapo wengi sana, ila bado hatujapata ushahidi wa kuweza kuwataka hadharani.”
Read more ...

LAANA...!! MJAMZITO ASALITI NDOA, AJIFUNGULIA GESTI AKIWA NA MWANAUME MWINGINE


MJAMZITO wa miezi saba Bi. Mwanaidi Athumani mkazi wa Chamwino Morogoro hivi karibuni alifanya mchepuko wa kutoka nje ya ndoa na kujikuta akijifungua mtoto wa kiume ndani ya gesti iliyopo maeneo ya Mafisa mjini hapa, 

Habari zinasema kuwa mwanamke huyo alifanya mchepuko huo baada ya mumewe kusafiri kwenda kutafuta fedha za maandalizi ya kujifungua kwake.

Bila ya kujali kama ana mimba ya miezi saba, Mwanaidi aliingia katika gesti moja (jina tunalo) akiwa na mwanaume anayedaiwa kufanya kazi ya kupiga debe katika stendi ya Msamvu na mambo yalipomwendea kombo, mwanaume huyo akatimua mbio.

Kwa mujibu wa shuhuda wetu, Mwanaidi na mpiga debe wake walipanga katika chumba namba 3 na baada ya kufanya mambo yao, Mwanaidi akaanza kupiga kelele kutokana na kushikwa na uchungu. Ilimbidi mhudumu wa gesti hiyo, Bi. Moshi Eliya afike kumsaidia Mwanaidi aweze kujifungua salama pamoja na kwamba hakuwa na ‘gloves’ wala kitu chochote cha kulinda afya yake.

Chanzo chetu ambacho nacho kilikuwa ni mpangaji ndani ya gesti hiyo kilisema kuwa tukio hilo lilitokea saa 8 usiku na Mwanaidi alipiga kelele huku akizozana na mpiga debe wake. 

Kiliposikia tukio hilo, chanzo hicho kikapiga simu kwa paparazi wetu aliyetinga katika nyumba hiyo ya wageni kwa ajili ya kushuhudia tukio hilo.

Baada ya kujifungua salama, paparazi wetu alimuuliza Mwanaidi kilichotokea ndipo mwanamke huyo akafunguka kuwa alikuwa amechepuka nje ya ndoa baada ya kukumbwa na shetani.

“Nina mume na tuna watoto watatu huyu ni wanne, mume wangu amesafari kwa ajili ya kutafuta fedha za maandalizi ya ujuo wa mwanetu akijua nina mimba ya miezi saba,” alisema mwanaidi. Pamoja na kutaka kugoma, lakini mwandishi wetu alimchukua mwanamke huyo na kichanga chake na kuwapeleka Hospitali ya Mkoa wa Morogoro ambako wamelazwa kwa uchunguzi zaidi.

Mhudumu wa gesti hiyo, Bi. Moshi Eliya ambaye alikuwa mkunga wa Mwanaidi alisema kuwa alishindwa kutumia ‘gloves’ wakati wa kumzalisha mzazi huyo kwa kuwa alikumkuta mtoto ameshaanza kutoka. “Mtoto aliashaanza kutoka, hata hivyo kwa usiku ule tungepata wapi hizo gloves?” alihoji.
Read more ...

NDEGE YA MH370 YA MALAYSIA ILIBADILI MKONDO

Ndege ya Malaysia iliyotoweka
Mkuu wa jeshi la anga la Malaysia, amekanusha madai kuwa ndege ya Malaysia iliyotoweka, ilionekana mara ya mwisho Magharibi ya rasi ya nchi hiyo, eneo ambalo ni mbali zaidi na njia iliyostahili kupita.

Generali Rodzali Daud, amesema kuwa hawawezi kupuuza uwezekano huo, lakini amesema madai kuwa mawasiliano ya ndege hiyo yalinaswa na mtambo wa radar katika eneo hilo sio kweli.

Amesema mawasiliano ya mwisho ya ndege hiyo iliyokuwa ikitoka Kuala Lumpur kuelekea Beijing yalinaswa katika rasi iliyoko kati ya Malaysia na Vietnam.

Ndege na meli kadhaa zimekuwa zikitafuta mabaki ya ndege hiyo katika eneo la bahari ya Malaysia, lakini hazijafanikiwa kupata mabaki ya ndege hiyo.

Msako unaendelea

Jeshi la Malaysia limesema kuwa, mtambo wake wa radar unaashiria ndege hiyo iliyotoweka, ilielekea eneo la Magharibi, mbali na njia iliyostahili kupita kabla ya kutoweka.

Ndege hiyo MH370 ilitoweka siku ya Jumamosi, baada ya kupaa ikiwa na abiria mia mbili na thelathini tisa.
Juhudi za kimataifa za kutafuta ndege hiyo zimepanuliwa na kuimarishwa.

Awali ilibainika kuwa watu wawili waliokuwa wakisafiri kwa kutumia paspoti zilizoibiwa walikuwa raia wa Iran ambao hawana uhusiano na kundi lolote la Kigaidi.

Ndege ya Malaysia iliyotoweka kabla ya kutoweka siku ya Jumamosi
Read more ...

MASKINI....!! WEMA SEPETU ALIA KUTOPATA MTOTO, MSIKIE HAPA AKIFUNGUKA.

MASKINI! Kilio kikubwa cha Wema Isaac Sepetu ni kupata mtoto, Risasi Mchanganyiko linafunguka.
Habari zilieleza kuwa Wema amekuwa na kiu ya mtoto kwa muda mrefu na kwamba alishakuwa na wanaume tofauti lakini hawakumpatia mtoto.

Ilisemekana kwamba katika msururu wa wanaume aliominya nao kimalavu, iliwahi kuripotiwa kuwa ni mwanaume mmoja tu aliyefanikiwa kumpa ujauzito lakini kwa bahati mbaya mimba ilichoropoka.

Mwanaume aliyekuwa na mzigo huo ilidaiwa ni Prezidaa wa Bendi ya Mashujaa Musica, Charles Gabriel ‘Chaz Baba’.

Baada ya kupania kwa muda mrefu bila mafanikio, ilidaiwa kuwa mwanadada huyo mkali wa sinema za Kibongo aligeuzia mapenzi yake kwa mbwa (pets) wake wawili, Van na Gucc ambao mmoja wao amezaa hivi karibuni.

Habari zinadai kuwa, kutokana na mapenzi yake na mbwa hao, amekuwa akiwagharamia mkwanja mrefu katika chakula na shopping za mavazi ya bei mbaya.

WEMA ANAFAFANUA
“Nawapenda sana mbwa wangu, nawaona kama ndiyo watoto wangu kwani sina mtoto na ninatamani sana ila najua Mungu atanijalia siku moja muda ukifika,” alisema Wema na kuongeza:
“Kila jambo na wakati wake, nitapata tu, nadhani ni suala la muda tu. Watu wanaweza kushangaa namna ninavyowapenda mbwa wangu, nawathamini kwa sababu wananipa faraja na nipo nao karibu. Nawajali kama binadamu.”
Kabla ya Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ anayetoka naye kwa sasa, wengine waliowahi kuonja penzi lake na wakashindwa kumpatia mtoto ni pamoja na marehemu Steven Kanumba, Jumbe Yusuf na Chaz Baba.
Read more ...

NYUMBA YA MSANII WA FILAMU ZA KIBONGO "SALADINI" YATEKETEA KWA MOTO

Ashura Rashid ‘Saladini’.
NYUMBA ya msanii wa filamu za Kibongo aliyewahi kutamba na muvi kali ya Saladini, Ashura Rashid ‘Saladini’ imeteketea kwa moto na kusababisha hasara kubwa, huku msanii huyo akihaha kusaka hifadhi kwa majirani, Chande Abdallah anakujuza.
Tukio hilo lilitokea asubuhi ya Machi 6, mwaka huu maeneo ya Bugando jijini Mwanza wakati msanii huyo akiwa kwa majirani zake ambapo chanzo cha moto huo kilidaiwa kuwa ni hitilafu ya umeme.
Akizungumza na Showbiz kwa njia ya simu, Saladini alisema kuwa kwa sasa analala kwa majirani kwa kuwa kila kitu chake kimeteketea kwa moto.
“Namshukuru Mungu hakuna aliyedhurika lakini nimepata hasara kubwa sana kwani hakuna kitu kilichotoka salama humo ndani,” alisema Saladini kwa masikitiko
Read more ...

HAPANA CHEZEA VIROBA...!! TAZAMA MENEJA WA CLUB ALIVYOTEPETA, VIROBA VYA KONYAGI VYAMFANYA MBAYA MENEJA HUYU.

 Meneja wa Club ya V.I.P mjini Iringa Mick akiwa  amezima baada ya kunya viroba na kisichana kwa  kuonyesha uwezo  wake na baada ya dakika 20 akazima kama hivi ,hapa nalazimika  kukumbuka ule ujumbe wa  chonde chonde! ulevi Nomaaaaaaaaaa!?


 Mlinzi  wa eneo la TFA akijaribu kumsaidia baada ya polisi kufika na kuamua kumwacha kutokana na ugonjwa wake wa pombe kutokuwa na daktari wa kutibu 

 
 Wasamaria  wema   wakimtazama meneja huyo chapombe akiwa amezima 
 Hapa idadi ya walinzi  ikiendelea  kuongezeka eneo la tukio mjini Iringa usiku huu 
Ukisema ulevi noma wapo watakaosema ulevi ni sehemu ya kupoteza mawazo ila kwa tukio hilo kila mmoja anaweza ungana nami kuwa kweli ulevi noma hapa ni eneo na TFA mjini Iringa ambapo meneja  huyu wa Club ya V.I.P akiwa amezima kwa kunywa pombe kupita  kiasi
Credit: michaelngilangwa.blogspot.com 
Read more ...
Designed By Blogger Templates