Saturday, April 19, 2025

Breaking News
>> DADA ZETU SIKU HIZI MNABOA SANA KWA HAYA MAVAZI YENU..!!  >> VIDEO : MWANACHUO AFUMWA AKICHEZA NUSU UCHI KWENYE MTANDAO WA SKYPE BAADA KUDANGANYWA NA MZUNGU ALIYEKUWA ANACHAT NAE...  >> MWANAFUNZI WA CHUO KIKUU NCHINI AJIUZA KWA KUWEKA PICHA ZA UCHI KWENYE PROFILE YAKE YA FACEBOOK   >> BAADA YA PICHA ZAKE ZA UTUPU KUSAMBAA, WATU WAMPA MAKAVU LIVE MISS TZ REHEMA FABIAN...  >> NAPENDA WAPENZI WA MTANDAONI ,ILA TUKISHA ''DO'' SIWAPENDI TENA...  >> Unajua athari za kuitana sweet, dear, baby katika mapenzi...?? SOMA HAPA NKUJUZE.    

Picha na habari kamili kuhusu vifo vya watu 10 vilivyosababishwa na na ajali ya basi la Allys na Bunda mkoani Mwanza


Watu kumi wamefariki dunia, wanane kati yao papo hapo na wengine 16 kujeruhiwa katika ajali mbili tofauti zilizohusisha mabasi ya kampuni ya Bunda na Ally, mkoani Mwanza.

Ajali hizo zilitokea ijumaa usiku katika barabara kuu ya Mwanza-Shinyanga katika maeneo ya Mitindo wilayani Misungwi na eneo la Buhongwa Dampo wilaya ya Nyamagana jijini Mwanza.

Ajali mbaya zaidi iliyosisimua na kusababisha vilio kuugubika mji wa Usagara wilayani Misungwi, ilitokea majira ya saa 1:40 Buhongwa, ambapo Basi la Allys lenye namba za usajiri T.691 AGP liligonga Daladala (Toyota Hiace)na kusabaisha vifo vya watu tisa ambao kati yao, saba walikufa palepale. 
Mwonekano wa dalaldala kwa nyuma. 
Kamanda wa polisi mkoani Mwanza, Valentine Mulowola akithibitisha ajali hiyo, alisema basi hilo lililokuwa na hitilafu ya taa za mbele, lilikuwa likitoka Arusha kwenda jijini Mwanza wakati daladala hiyo ikitoka Buhongwa kwenda Usagara wilayani Misungwi.

Baadhi ya abiria waliokuwa katika ajali hiyo akiwemo Shija Francisco ambaye alijeruhiwa mkono wa kulia alisema kuwa ,basi hilo liliwagonga sehemu ya ubavu wa kulia na kusabisha Hiace hiyo ipinduke na kuviringika mara tatu nje ya barabara, wakati likijaribu kulipita roli moja lililokuwa mbele yake kwenye kona.

 “Ilikuwa ghafla mno tulipojikuta uso kwa uso na basi hilo ambalo halikuwa na taa, dereva akajaribu kulikwepa lakini hakufanikiwa, lilitugonga na kufanya gari letu lipinduke na kuviringika mara tatu.” Alieleza Franchisco mkazi wa Usagara huku akimlilia mkazi mwenzake Juma Basu (27) aliyekufa papo hapo.
  
 Usiku huo wa ajali ilishuhudiwa miili ya watu hao ambayo baadhi ilikuwa imepondeka vibaya na kukatika viungo akiwemo mtoto wa miaka minne, Raphael Simon aliyekufa pamoja na baba yake Simon Paschal(35), wakazi wa Usagara.
  
 Kamanda Mulowola aliwataja wengine waliokufa katika ajali hiyo kuwa ni Eliakim Fredrick mkazi wa Igogo Mwanza, Stephen Mungisa (hatambulika makazi), Dismas Mpange (Usagara)na wanawake wengine wawili ndugu Shobo Lumecha na Gaudensia Lumecha, wakazi wa Geita. 
  
 “Abiria 15 walijeruhiwa katika ajali hiyo akiwemo dereva wa Hiace Anthony Maige (52) na kukimbizwa katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando lakin dereva wa Basi la allys Elias Charles alikimbia,  tunamsaka.” Alieleza Kamanda huyo na kubainisha kuwa daladala hiyo ilikuwa imejaza watu kupita kiasi.

Basi la Ally's lililoigonga daladala na kusababisha vifo vya watu 9.

Basi la Bunda Express lililomgona mwendesha baiskeli.
 **
Katika ajali nyingine iliyotokea jana saa 11 jioni katika eneo la Mitindo Misungwi, Basi la Bunda T.234 BZK aina ya Scania likiendeshwa na Emmanuel Mashauri, limemgonga mwendesha baiskeli Shilaga Thomas (20) na kusabaisha kifo chake palepale na kumjeruhi abiria wa baiskeli hiyo Machwenda Komanya.

Kamanda Mulowola amesema kuwa chanzo cha ajali hiyo ya basi la Bunda lililokuwa likitoka Dodoma kwenda Musoma, ni mwendo kasi na ametoa wito kwa madereva kuwa waangalifu.

<<GSENGO >>
Designed By Seo Blogger Templates