Breaking News

MADEE AITAJA SIRI YA MAFANIKIO YAKE "NIMEGUNDUA SEHEMU GANI NILIKUWA NACHELEWA"...MSIKILIZE HAPA

madee  

Hitmaker wa ‘Sio Mimi’ Madee, amesema kabla ya kuachia ngoma hiyo iliyompa mafanikio makubwa mwaka jana, alikuwa hajaigundua siri ya mchezo na sasa hawezi kurudia tena makosa aliyoyafanya mwanzo.

 Madee amesema mwaka jana aligundua ni wapi alipokuwa akikosea.

Unajua kuna aina ya muziki ambao mimi nilikuwa naufanya nyuma kabla ya huu muziki ninaoufanya sasa hivi, nadhani aina ya huo muziki una wapenzi wengi sawa watu wanaupenda, lakini wale wanaoupenda ule muziki sio wanunuaji ni vijana na unajua vijana mara nyingi wao michongo yao hawanunui nyimbo, wanaburn.

 Huu muziki ambao nimeingia sasa hivi nawashika rika zote kuanzia watoto mpaka mababu kwahiyo inakuwa rahisi mimi kufanya biashara, kokote nasikika, kuanzia mtaani, redio, club, inakuwa rahisi mimi kupenda.”

Katika hatua nyingine, Madee amesema video ya wimbo wake ‘Tema Tuwachape’ iliyofanywa na kampuni ya Ogopa itatoka mapema mwezi huu.

 Pia aliongeza kuwa mwezi February ataachia wimbo mpa uitwao Shneida.

credit: bongo5
Designed By Blogger Templates