Mashuhuda wa tukio hilo pamoja na wahudumu wa bar ya Bulls park wakimuangalia msela huyo akiwa hajiwezi kwa lolote baada ya kuzidiwa na ngano a.k.a maji ya Ilala.
Ama kweli Pombe sio Chai,cheki jamaa alivyosherehekea krismas
Kijana mmoja ambaye jina lake halikuweza fahamika mara moja alijikuta akipiga mweleka wa nguvu na kushindwa kunyanyuka kwa kile kinachosemekana kwamba alizidiwa na pombe.
paparazi wetu alifika eneo la hilo mda mchache baada ya kutokea na kumshuhudia kijana huyo akiwa amelala chini pasipo kujiweza,huku Wasamaria wakionekana kujaribu kumwagia maji ili aweze kurudi katika hali ya kawaida pasipo mafanikio.
Baadae kidogo alijitokeza kijana mmoja na kukiri kuwa ndiye aliyekuwa akistarehe na mshkaji wake huyo na wakati wa kuondoka alimkabidhi kwa dereva bajaji mmoja ili amfikishe mahala anakokwenda na yeye kurudi ndani na kuendelea kugonga zake moja moja,kumbe huku nje jamaa hakufanikiwa kupanda ile Bajaj na kujikuta amedondoka na kuulala hapo hapo.
Kijana huyo pia alisema kuwa kijana mwenzake alikuwa ni mwenyeji wa Mwanza na alikuja Dar es Salaam maalum kwa ajili ya kula bata a.k.a kujirusha katika kipindi kiki cha sizoni ya sikukuu za krismas na mwaka mpya na nayeye na ndipo akakutwa na huo mkasa.