Breaking News

NIMEGUNDUA MUME WANGU NA MIMI NI NDUGU WA DAMU KABISA...!! USHAURI JAMANI



Habari wadau wa Mnyetishaji
Mimi na mume wangu tumefunga ndoa siku si nyingi , hapa tulipo tumechanganyikiwa sababu tumegundua sisi ni ndugu wa damu.....!!

Story nzima ipo hivi ...!! Mimi nimelelewa na mama angu tu baba angu alinikataa nikiwa mdogo na akahama nchi kwenda kuishi Marekani ...so mimi na mama hatukuwa na mawasiliano naye kabisa mpaka naolewa hata baba hakuusika katika shughuli...


Basi juzi kati amerudi Tanzania na akakutana na mama angu na mama akamwambia nishaolewa ...so akataka kuja kunisalimia mimi na mume wangu ...alivyofika tu nyumbani kwetu mume wangu akampokea kwa furaha zote na kumsalimia.


Baada ya maongezi mengi BABA aliniita pembeni na kunieleza kuwa yule mume wangu ni kaka yangu wa damu na alizaa na mwanamke mmoja baada ya kuachana na mama yangu..
Hapa nilipo nimechanganyikiwa sijui hata nifayaje...??? Sijui nimuelze mume wangu ukweli...?? NAOMBENI USHAURI JAMANI SIJUI NIFANYE NINI....
Designed By Blogger Templates