Hitmaker waPesa, Mr Blue aka Kabayser amesema tangu awe baba, maisha yake yamebadilika na haishi kama zamani tena.
Mr Blue na mwanae Sameer
“Nafikiri kwa mimi imenikuza zaidi,” Blue ameiambia paparazi.
Hata hivyo amesema pamoja na kuwa baba, majukumu aliyonayo hayajabadilika sana japo kwa sasa amekuwa yeye binafsi na familia yake. “Kilichobadilika kwangu ni bidii kuongezeka inabidi niangalie familia yangu iandaje.”
Wahyda (mchumba wake na Blue) akiwa na mwanae Sameer
“Ni mtu kwakweli kama baba yake na mimi nafurahi,” Blue amemuongea mwanae huyo wa kiume aitwaye Sameer. “Inabidi amrithi baba yake tu kwa uchakarikaji na kila kitu.”
Wahyda
Katika hatua nyingine Mr Blue amesema tayari amemalizia mjengo wake na anatarajia kuhamia tarehe 1 January 2014.